slide show

Thursday, May 2, 2013

USOME WASIFU WA TOX STAR OR BONGO FABOLOUS OR KING OF PRETTY GIRLS TOKEA GREEN CITY


Jina kamili; Juma Saidi
A.k.a; Tox Star or Bongo Fabolous


Home;  Mbeya City
Tarehe ya kuzaliwa;   25 January
Shule;   Iyunga Primary school na Iyunga Sec School
Style ya Muziki;   Muziki wowote
Kazi nyingine nje ya Muziki;  Balozi wa Maduka ya Hussein Pamba Kali
 (Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla)

 Ofisi ya Tox Star ambayo yeye ni Balozi wa hii crib ya Hussein Pamba Kali

Label ya Muziki; Hana Lebo ila kazi zake nyingi huzifanyia Sharobaro Records

Mahusiano;   Hajaoa bado au unaweza kusema bado yupo yupo saaaaaaaaaana
Kipaji kingine;   Basketballer na Ni Uigizaji wa Filamu,
Baadhi ya filamu ambazo
Tox Star ameshashiriki ni Kama ''Watoto wa Mjini'' na ''Tanzania to
 Denmark'' ambayo ameshirikiana vyema mwanadada Lucy Komba

Familia; Tox star ni mtoto wa nne kati ya watoto watano wa Mzee Saidi
 Nyimbo iliyomtambulisha kwenye Muziki wa Bongo ni Pretty Girl
 aliyomshirikisha Ally Kiba
nyimbo hii pia ilitengenezwa  Sharobaro Records, chini ya Bobby Joniour na 
Prodyuza wa video ni Abrah de Producer wa Golden Heart Studio (GHS)


Mangwea na dully sykes hawa ndio wanamuziki wanaomvutia zaidi Tox Star
pia katika nyimbo mpya iitwayo naomba unielewe amemshirikisha Mtoto
 wa Kariakoo Dully sykes


Kwa upande wa wasanii wa kike hapa Tanzania Tox Star huvutiwa na
Komandoo pia Shujaa Lady Jay Dee


Kwa upande wa Afrika mashariki Tox Star anavutiwa mno na Mkali aliyeimba Mpita njia
Alicios 



Kwa upande nje ya Tanzania Tox Star huvutiwa na Rapper Fabolous

 Matarajio ya baadae ya Tox Star ni kuwa mwanamuziki wa kimataifa ambapo
 amejipanga kuwashirikisha wasanii mbalimbali wa afrika mashaiki na kati
ambapo kwa kuanza amefanya kazi na M zambia aitwae Mr Rango kazi
hio ameifanyakatika studio iitwayo Green Record iliyopo nyumbani
Mbeya city chini ya Producer aitwae Gachi Boy

Alipoulizwa ni kwanini wasanii wengi wa Mbeya hukimbilia Dar na kupotelea huko?
alijibu kuwa yeye yupo tofauti sababu muda mwingi yeye huutumia akiwa Mbeya
hata nyimbo yake mpya itakayofata baada ya hii mpya ya ''Naomba unielewe''
aliyomshirikisha Dully Sykes ameitengenezea jijini Mbeya, na ndio nyimbo
aliyoshirikiana na mzambia aitwaeMr Rango pia akasema kuwa Vyombo vya
habari vya Dar es salaam havina ubaguzi ktk kucheza kazi za wasanii
wa pale Dar pia mikoani
tofauti na ilivyo Mbeya ambapo kazi za wasanii wa Mbeya
 zinazotengenezwa Mbeya hazipewi
airtime pia promo ya kutosha kama ilivyo Dar es salaam ambako Tox Star
amesema kuna connection kubwa ya kufanikiwa tofauti na Mbeya,
pia akawaomba wadau wa Muziki Mbeya wawe wazalendo na wathamini
cha nyumbani kwanza ili kuliinua jiji kisanaa pia kufanya sanaa ya muziki
kuwa kazi ya kuwaingizia vipato wanamuziki wa Green city
kwa ushauri au lolote jingine unaweza kumpata Tox Star ktk ukurasa wa
wa facebook kwa kusearch jina Star Tox au unaweza kumpata kwa
ku like page yake ya facebook anayotumia jina la Tox Star



2 comments:

comments

***