slide show

Tuesday, February 19, 2013

HUYU NDIE WALTER CHILAMBO a.k.a SPEECHWISE, MWANA RnB wa KWANZA WA KIUME KU SHINE BONGO TOKEA GREEN CITY (MBEYA CITY)



            Jina kamili:Walter Chilambo a.k.a Speechwise

Nyumbani; Mbeya City
Tarehe ya Kuzaliwa: 13/March
Kazi: RnB Musician (Bongo flavour) (Epiq Bongo Star search_Zantel)
Kipaji kingine: Music production/Producer
Elimu: O-Level / Sangu Secondary School/Mbeya Tanzania
Role Model; Keneth Brian a.k.a  BabyFace
Prodyuza wanaomvutia duniani: Swizz Beatz na Peter Todd


                              Hapa akiwa na mshiriki mwenzie wa EBSS akisubiria
                               kutangazwa kama mshindi wa EBSS 2012

 Moja kati ya siku ambazo Nyota Walter Chilambo hataja kuzisahau
 maishani mwake


Hapa akitabasamu baada ya kushinda milioni 50 za kitanzania katika  
mashindano EBSS yaliyofanyika mwaka 2012


Huyu ndie mtu mzima  Kenneth Brian au BabyFace ambaye ni mzawa wa 10/april/1958
 huko Indianaambaye ndie Role Model wa Walter Chilambo, kwa upande waimbaji
 bora wa RnB hapa Duniani

Licha ya uimbaji kipaji kingine cha Walter Chilambo ni U prodyuza 
na Swizz Beatz Pichani juu
 na pia
Prodyuza wa Zomba Records ya US aitwae Peter Todd ni moja kati 
ya prodyuzaz  wanamvutia mno Walter Chilambo,

Kwa upande wa familia ya Walter Chilambo ipo kama ifuatavyo
Yeye ni Mtoto wa pili katika familia ya watoto watatu, nimebahatika kulelewa na
 mama na baba mlezi jijini Mbeya, kwa sasa nipo Dar aliko 
Baba yangu mzazi pia nafanya kazi  zangu huku nikiwa naishi mwenyewe.

Nimemalizakidato cha nne mwaka 2009 na matokeo hayakuwa 
mazuri na kuamua kuanza kujishughulisha rasmi na kazi za Muziki
na mwaka 2011 nilikuja Dar rasmi kwa ajili ya shughuli hizo.

Baada ya kufanya kazi kidogo mwaka jana (2012) nikashiriki 
mashindano ya vipaji vya  sanaa ya muziki Epiq Bongo Star Search 
na Mungu akanisaidia nikawa mshindi wa mashindano hayo.

Ushindi wa Epiq BSS Umekuwa mwanzo wangu mzuri wa mafanikio 
katika kazi zangu za 
muziki na maisha kwa ujumla kwani kwa sasa nafahamika pia 
zawadi ya Sh. 50. Mil imenisaidia sana.

Najua sasa ni moja kati ya wasanii wa Tanzania ambapo 
nategemea kuendelea kufanya
 kazi nzuri na kukufanya wewe shabiki yangu kuendelea 
kuwa na mimi na kunipenda tangu 
umenifahamu, Nakushukuru sana na naomba tuendelee 
kuwa pamoja katika kazi zangu.
Mwaka huu Walter Chilambo ameibuka na single ya kwanza iitwayo 
''Siachi'' ambayo pia 
ameonyesha upendo
kwa kumshirikisha Mrembo mwenye kipaji cha hali ya juu pia 
kutoka THT aitwae Vida,
 ambaye amesikika kwa mbali katika back vocals za wimbo wake
 uitwao ''Siachi''

                             Hapa akiwajibika jukwaani siku ya fainali ya EBSS Kulia
 ni mwanamuziki Ben Pol 
              akimtuza baada ya kukoshwa na uwezo adim wa Walter Chilambo
               a.k.a Speechwise
              
               Mwisho Walter Chilambo anawaomba wapenzi wa muziki 
Tanzania, muzipokee 
              yake mpya  iitwayo ''SIACHI"' pia kazi zake nyinginezo
 zitakazofata baada ya hii,
                Mungu akubariki wewe unayesoma haya maelezo kuhusu
 Walter Chilambo

No comments:

Post a Comment

comments

***