slide show

Monday, January 28, 2013

HUYU NDIE ADILI MKWELA, a.k.a HISABATI a.k.a MAGAZITO a.k.a ALLEN IVERSON a.k.a THE MAGNETIC PARM



Jina Kamili,Adili Mkwela a.k.a Hisabati au Magazijuto, 
Mzaliwa wa November 26, Asili yake ni Mjini Mbeya,




Katika familia ya Bibi na Bwana Mkwela Adili ni mtoto
 wa tano kati ya watoto sita, ambapo katika familia yao
 kuna watoto wa kiume wanne na wakike wawili,

Tangia anakua adili alionyesha kipaji kikubwa 
ktk mchezo wa kikapu (Basketball) na Muziki pia

 Uwezo wake ulianza kuonekana rasmi Alipofanikiwa
kuanza kushiriki mashindano ya kitaifa ya mpira wa 
kikapu hapa Tanzania, Kutokana mna vitu adimu
 alivyokuwa akivionyesha 
awapo dimbani mashabiki walimbatiza jina la 
utani (ALLAN IVERSON)




Juu ni Picha za Allen Iverson akiwa katika pozi tofauti

dimbani Mashabiki hao wakawa wanamlinganisha
 na mchawi kikapu kutoka ligi kuu
ya mpira wa kikapu nchini Marekani aitwae Allen Iverson,
 na pia wakamuongeza jina lingine kwa kumwita
 Magnetic Parm yote ni kwa sababu ya uwezo wake 
wa kumiliki mpira uwapo katika mikono yake pasipo
 kuupoteza mbele ya wapinzani wake, 

Kwa upande wa muziki alimvuta kuupenda na hata 
kuvumbua kipaji chake ni Kaka yake aitwaye Adam,
 Ambaye alikua akimsikilizisha kazi mbalimbali za wasanii
 kama
KRS ONE
Juu ni 
Father of Hiphop KRS ONE
Nas Escoba

Hali iliyopelekea mwaka 2002 kufanikiwa kurekodi
nyimbo yake ya iliyomtoa kwenye game la Bongo
 fleva, nyimbo hii aliwashirikisha wasanii kutoka
 Arusha ambao Mandojo na Domokaya,
Juu ni Mandojo na Domo kaya walioimba kiitikio cha 
wimbo 
uliomtambulisha Hisabati (PEKE YANGU)

Pia nyimbo hii ilifanikiwa kuchaguliwa na Redio
one, BBC Music Awards na pia kama wimbo bora
wa hiphop kwa mwaka 2003, Baada ya hapo
Adili alitengeneza kundi lililoitwa CHOKA MBAYA 
Ambamo ndani yake alikuwemo Gwiji wa 
Muziki wa Hiphop Tanzania Professor Jay,



The Heavy weight Mc Katika pozi

Baada ya hapo alifungua kampuni yake binafsi 
mwaka 2004, iliyoitwa Chapakazi, iliyojihusha na 
kurekodi Sauti na Video pia Kampuni hii ilichaguliwa 
katika tuzo za muziki za Kilimanjaro MWAKA 2006





pia Adili Mkwela alishiriki katika album ya pamoja akiwa mmoja
wa wanaharakati wanaopigania ukombozi wa Hiphop na 
sanaa kwa ujumla YA Tanzania
]

2 comments:

  1. UMOJA NI NGUVU
    UTENGANO NI DHAIFU
    TUMEAGIZWA UPENDO
    TUPENDANE
    pansullah chavichavi

    ReplyDelete
  2. Ngoma yake mpya tunaipataje

    ReplyDelete

comments

***