slide show

Friday, April 5, 2013

TEGUA UTATA WA MUDA MREFU KWA KUUFAHAMU KIUNDANI MUUNGANO WA MBEYA ALL STARZ FROM GREEN CITY


JINA LA KWANZA MBEYA OLD SKU STARZ AU MBEYA ALL STARZ
KUZALIWA KWA KUNDI;2011 MAY, MBEYA CITY
MUANZILISHI; BENJAMINI MBILINYI (DJ DIZZO THE PRACTICAL SKILLZ)
Ambaye pia ni Prizenta wa Highland fm 92.7fm Mbeya
HIT SONGS; Mbeya Our Home, Tusaidie (2011 JULAI na November 2011
ikatengenezwa nyimbo iitwayo Hiphop zote Zilitengenezwa na 

Michael Ndibalema a.k.a Prodyuza Losso, katika studio iitwayo Mashada Inc Production

Picha ya Prodyuza Losso ktk Pozi
Baada ya hapo mwaka 2012 julai Mbeya All Starz walitoa wimbo ulioitwa ''Mbeya Nyumbani''
ambao ulifanywa na Prodyuza Zest akishirikiana na Rash Don wa Mojamoja Records

Prodyuza Zest

Historia Fupi ya Muungano Huu ilianzia mwaka 2011 MAY 10 Ambapo Dj Dizzo au 
Benjamini Mbilinyi a.k.a Dj Dizzo The Practical Skillz ambaye ni Dj Mkongwe 
pia Prizenta wa Redio iitwayo Highland Fm 92.7Fm 

Dj Dizzo wa kwanza kushoto akiwa na wafanyakazi prizentaz wenzake

 Ambapo aliuanzisha Muungano huu kwa 
Jina la Mbeya Old sku Starz ambapo liliunganisha wasanii wa zamani wazawa
 wa Mbeya na baadae jina likabadilishwa baada ya kuona kuwa kuna umuhimu 
wa kuchanganya na wasanii wapya ili kuweza kuchanganya radha ambapo 
wakateuliwa wanaojulikana ndani ya Mbeya halafu likatengenezwa
 jina jipya la Mbeya All Starz

Mbeya Old sku 2011 May 
 Mbeya All Starz ktk moja ya picha zao

Muungano huu ulikua ukiongozwa na Mwenyekiti wa kundi aitwaye 
Gwanongwa Mwakasala a.k.a Mashetani ambaye amejing'atua ktk safari ya
 wanaharakati hawa mwezi wa 11 mwaka2012 na kuwaachia katibu wake aitwaye
Elifazi Mtwale a.k.a Doctor Fazi na Mhasibu wa kundi aitwae Miraji Hassan
au Zimwi Zivuva, 
Kwa mujibu wa muanzilishi wa muungano wa wasanii hawa Dj Dizo na mnukuu
 ''Mbeya All Starz ipo kwa ajiri ya Kuinua vipaji vya wasanii kutoka 
Mbeya City hasa vipaji vipya pia kuwaamsha wale waliokata tamaa na kuwa
kimya ilhali vipaji wamebarikiwa na uwezo mkubwa wanao
 pia kulibadilisha jiji la Mbeya kwa ujumla 
katika sekta ya burudani na kuifanya sanaa ya Muziki kuwa chanzo cha kipato 
kwa wasanii hawa ambapo huu Muungano huu huteua wasanii wenye
 vipaji na kuwafanyisha collabo ili kuongeza uzito na thamani ya nyimbo
 za wasanii kutokaMbeya City nje na ndani ya
Mmoja wa viongozi wa kundi hili alipoulizwa ni kwanini katika wasanii 
wanaosikika ktk nyimbo za Mbeya All Starz si wale wakubwa na maarufu waliopo 
Dar es Salaam, alijibu kwa kusema Mbeya All Starz maana yake
 watu (maarufu wa Mbeya) na si watu Maarufu wa 
Tanzania kundi hili lilipoanza mwaka 2011 May lilianza na wasanii hawa
 wanaojulikana hapahapa Mbeya na si hao wakubwa waliojulikana
 Tanzania hata hivyo aliongeza pointi moja kuwa hakuna kikwazo
 kwa msanii yeyote mzawa wa Mbeya awe anayechipukia au maarufu
anayehitaji ku show Love kwa kujiunga
 na huu Muungano uliodhamiria kulibadilisha jiji la Mbeya kiburudani,
 
               
     
 kuna wasanii wengi wanaounda kundi hili ambalo lina waimbaji wa 
kike wa3 ambao ni
First Lady Amychiba, Silvia na Junaisaty wasanii wa kiume ni kama Zimwi Zivuva, 
Anno Mellody, Zest Mkali, Doctor Fazi, Sanluu, Jay P, Shadamo, KD, D-Brain, 
Festo G, Danzi, Raymond, Nevy D, DrKiller, Sanu,Stimo, Mwaitege, Dayo, BZQ,
Nas E, Pc Ze Master, Zax B, Chant B, Joz B, Jacky Magic, Issa Dubert na wengine
kibao
Nyimbo Nyinginezo zilizorekodiwa na Mbeya All Starz ni kama 
Party Juu - Produced by Producer Effector aliyekuaga East Coast Team ktk
studio yake mpya iliyopo Mbeya iitwayo Zion Records iliyopo Block T,  Mbeya,
Salamu kutoka Mbeya By Prodyuza Zest Mkali na We Make More Better
iliyotengenezwa na Moh Mocko wa Mashada inc

Baadhi ya Malengo na Mafanikio ya Mbeya all Starz ni kufanikiwa kushawishi
wakazi wa Mbeya pia vyombo vya Habari vya Mbeya kutoa sapoti kubwa kwa wasanii
 wa Mbeya ambapo kwa sasa mambo yamebadilika si kama zamani,
Pia Mbeya All Starz w kwa kushirikiana na wadau wakubwa wa sanaa Mbeya
wapo ktk
 hatua za Mwisho za kuanzisha Organisation iitwayo UWASAMBE au
UMOJA WA WADAU WA SANAA MBEYA,
ili kuweza kuiinua sekta ya Sanaa kwa Ujumla Mbeya,,
Mwisho Kiongozi wa Mbeya All Starz aliihusia Serikali ya Tanzania kuwekeza
 kwa vijana kwa kuwasaidia ktk kujiajiri na kuifanya sanaa kama ajira na
 kuipunguza idadi ya vijana waliokosa ajira Tanzania





8 comments:

  1. ipo sawa..keep t' rockin

    ReplyDelete
  2. Big up guys, make it real. Mbeya city stand up






    ReplyDelete
  3. Tatizo lenu ni wabinafsi sana hamtaki kushirikiana na wasanii waliowazidi uwezo japo hawajapata nafasi...msanii kama Myahudi,Chaz kidalipoo,Seif cash,KB,Joviarry,Ackarius,Nolesy,Nest west,Elvics,Fancy,Baby chio,K-joh,Ryder boy,Clarence,D-twice na wengine kibao mnawaonea wivu mnahisi watawafunika...acheni ubinafsi na ikiwezekana muwatafute hao wasanii haraka sana LA SIVYO hakuna atakayewasapoti

    ReplyDelete
    Replies
    1. KIJANAHAO ULIOWATAJA HAPO KUNA AMBAO VIWANGO BADO KABISA NA MBEYA ALL STARZ NI YA WANA MBEYA WOTE KTK HIO LIST KB YUMO MBEYA ALL STARZ PIA NOLESY, WALIONGEZWA 7BU NI KWELI WANA UWEZO KWELI NYIE WENGINE FANYENI MAZOEZ ZAID OTHERWISE MTAENDELEA KUSUGUA BENCHI

      Delete
  4. Respect and I have a tremendous offer: How Much Full House Renovation Cost house renovation tax deduction

    ReplyDelete

comments

***