Monday, June 10, 2013

IFAHAMU TAREHE AMBAYO VIDEO YA MBEYA ALL STARZ ITAFANYIKA KAZI NA MPANGO MZIMA UTAKAVYO KUWA


Baada ya kusumbua na wimbo wa Mbeya Nyumbani 
na Salamu toka Mbeya huu ndio ujio mpya wa 
Mbeya all starz, ambapo kwa sasa wataanza na Video
halafu itafata audio,Mpango mzima wa audio unafanyiwa ktk
studio mpya iitwayo G2G Records, chini ya Prodyuza Losso,
akishirikiana na Prodyuza Ahazi, japo kwa asilimia 90, mzigo
mzima unasimamiwa na Prodyuza Losso,


Kutoka kushoto ni Zimwi Zivuva, Doctor Fazi, Danzi, Sanluu, 
Producer Losso kabla ya recording  

Prodyuza Losso mna Producer Ahaz, wakimalizia editing ya 
wimbo mpya wa Mbeya all starz (Blessed) 
ambao upo ktk mahadhi ya tofauti mno
Pia wasanii wanahitaji ongezeko la Models wa video wa video ya 
Wimbo huu ambayo itafanyika tarehe
13 na 14 hapa jijini Mbeya chini ya Kampuni mbili za ambazo
ni Disturbing Tzee Video Company na Mashada Inc Videoz 

Doctor Fazi, Losso na Ahaz,
 
Kama wewe ni model na ungependa kushriki katika hizi video 2 
waweza kuwacheki watu wafuatao 
  http://www.facebook.com/Doctorfazi  - 0652384615,
au http://www.facebook.com/Concluder- 0654079930
au http://www.facebook.com/producerlosso -0768540772


Akiongea na Mwandishi wa Blog hii kiongozi kwa kundi hilo aitwaye
Doctor Fazi amesema ktk video hii watashirikishwa Ma Djz na
Watangazajiwa Redio zote za Green City pia Wadau wa 5 
wanaosapoti mno muziki wa Mbeya,

 Wasanii wa Mbeya all Starz ktk pozi, Mungu
 ibariki Mbeya, Mungu ibariki Tanzania

Monday, May 13, 2013

HUU NDIO UKWELI WA HISTORIA YA MBEYA CITY NA MAAJABU 13 YAPATIKANAYO GREEN CITY TU, NA SI POPOTE DUNIANI


 1.
Jina la Mbeya limetokana na neno la kisafwa "Ibheya"
ambayo maana yake ni chumvi kwani miaka mingi
wafanyabiashara walikuwa wanafika mahali hapo
kubadilishana mazao yao kwa chumvi.
Mji wa kisasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni
Waingereza mnamo mwaka 1927. Wakati ule dhahabu
ilianza kupatikana katika mlimani karibu na Mbeya hadi Chunya,
Ramani ya Tanzania ikilionyesha Jiji la Mbeya upande wa kusini mwa Nchi, ikumbukwe kuwa jina la utani la Mbeya City huitwa Green City au Jiji la Kijani, yote ni kwasababu ya Mazingira mazuri ya Kijani yaliyopo Jijini Mbeya


hapa chini ni kipande cha Ramani kikiuonyesha mkoa wa Mbeya pamoja na wilaya zake kadhaa,
Ramani ya Mbeya

2.
Hapo mwanzo eneo la Mbeya liliitwa Scotland ya Afrika,
sababu kuu ikiwa ni wingi wa Miinuko (Milima) Pia hali
ya hewa ya Mbeya iliyotawaliwa na Misitu ya kijani, Ifananayo
na ile iliyopo Magharibi mwa Africa Kusini, ambayo pia hufanana
na milima ya nchi ya Ulaya iitwayo Scotland,
Picha ya moja kati ya milima ya Scotland, (Barani Ulaya) unaweza
 kutizama ni namna gani kuna kufanana na Milima ya Mbeya City

 3.
Mkoa wa Mbeya ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania ikipakana
na Zambia na Malawi, halafu na mikoa ya Rukwa, Tabora,
Singida na Iringa. Kuna wilaya 9 zifuatazo: Mbeya Mjini,

.

Mlima Loleza uliojitokeza karibu na Mbeya Peak, ndio huonekana
kutokea Mbali pale unapoingia Mbeya Mjini,

4.
Mbeya ni kati ya maeneo yanayopendeza kabisa ndani ya
Tanzania ikiwa na sehemu za


Picha ya Ziwa Nyasa ambapo ndipo inapopatikana Beach Mno 
iitwayo Matema Beach kama ionekanavyo pichani

 5.


Uwanda wa juu wa
Uporoto, Uwanja wa Usangu ingawa haukufikiwa bado na utalii.

Historia inavyoonekana katika jiografia ya Mbeya
Mji ulianzishwa katika sehemu zinazoitwa bado Uhindini,
Uzunguni na Majengo. Mji ulipangwa kufuatana na kawaida
ya miji wa kikoloni ya Afrika ya Mashariki kuwa na sehemu tatu:
 • Uzunguni ni sehemu ya nyumba za Wazungu na karibu na
ofisi za serikali (District Officer, polisi, mahakama)
 • Uhindini ni mtaa wa biashara uliokuwa hasa
 mkononi mwa wafanyabiashara wenye asili ya Uhindi na

6.

 • Uwanja wa mpira wa miguu uitwao Sokoine,
 • Majengo kama sehemu kwa wafanyakazi Waafrika na familia zao. 
 •  
Makanisa ya kale kama ishara ya historia
Mahali pa makanisa ya kale panaonyesha ugawaji huu wa kihistoria:
 • Kanisa Anglikana iliyokuwa dhehebu rasmi la
Uingereza lipo chini ya Uzunguni na karibu na ofisi za
kiserikali (zinazoelekea siku hizi kuhamishwa kwenda
Foresti) kama Mkuu wa Mkoa na mahakama. Kanisa
hili ni jengo dogo kwa sababu lilipangwa kwa kundi
dogo la maafisa na wafanyabiashara pamoja na wakulima Waingereza wa Mbeya.
 • Kanisa la Moravian la mjini ambalo ni dhehebu la
Kikristo asilia la Mbeya liko Majengo iliyokuwa sehemu
kwa Waafrika. Kati ya Waingereza hawakuwepo Wamoravian.
 • Kanisa Kuu Katoliki lilihudumia Wazungu wachache

Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi ni wakristo, hasa wafuasi
Makundi makubwa mjini ni Wasafwa wenyeji na Wanyakyusa
waliohamia hapa kutoka Rungwe. Wanyakyusa ndio waliotangulia kuleta
Uluteri mjini.
Kuna pia msikiti kubwa na hekalu la Wahindu.

7.
Bonde la Usangu

8.

 Kimondo kilichoangukia Mbozi miaka mingi iliyopita
kina uzito wa Tani 12,

9.

Mbuga ya Kitulo 
Mawasiliano
Mbeya ni njiapanda ya njia mbalimbali muhimu: Barabara
kuu ya lami kutoka Daressalaam (850 km) hugawanya
hapa kwenda MalawiMsumbiji kupitia Tukuyu/Rungwe,
na kwenda ZambiaAfrika Kusini kupitia Tunduma/Mbozi.
Vilevile njia ya reli ya TAZARA hupita Mbeya kuelekea Zambia.
Kuna ghala kubwa kwa ajili ya mizigo ya Malawi inayofikishwa
kwa reli kutoka Daresalaam bandarini ikihamishwa kwa malori
kwenda Malawi hapa Mbeya.
10.

Stendi ya Treni ya Tazara,

11.
Mbeya imekuwa na uwanja wa ndege mdogo usiokuwa na
huduma ya kawaida kwa muda mrefu. Lakini kuna mipango
ya kujenga uwanja mpya huko Songwe zipatao km 40 kufuata
njia ya kwenda Zambia.

Uwanja wa Ndege Songwe 
Wakazi
Mbeya ni kati ya miji kumi mikubwa ya Tanzania. Idadi ya
wakazi imekadiriwa kuwa wapatao 280.000 katika mw. 2005.
Wengine mnamo 300.000 wanaishi katika mazingira karibu na
Mbeya mjini.
Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa
ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na
makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha
kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

11.


 Ziwa Ngozi lililo juu ya kilele cha milima ya Uporoto huko Rungwe,

Uchumi
Uchumi wa Mbeya mjini umetegemea kilimo cha mazingira yake
na biashara. Viwanda mbalimbali vilianzishwa lakini havikufaulu sana.
Kuna viwanda kwa mfano Zana za Kilimo, Highland Soap, Mbeya Textiles.
Mbeya Ceramics iliporomoka kitambo.
Tangu miaka ya 1990 kitovu cha mji kinahamishwa kutoka eneo
la zamani kwenda karibu na barabara kuu ya Daresalaam – Zambia.

13.
Picha 2 tofauti zikilionyesha Daraja la Mungu, ambalo
 ni halijatengenezwa na binadamu liliumbwa hivyo vivyo


Elimu
Pamoja na shule za sekondari kuna taasisi kadhaa za elimu ya juu kama vile:
cha Kanisa la Moravian Tanzania kinachotoa kozi za ualimu
na theolojia tangu mwaka 2005. Kilitanguliwa na chuo cha Motheco.
 • Mbeya Technical College
 • Chuo cha Kilimo Uyole (Agricultural Research Institute -ARI- Uyole)
 •  ambacho ni taasisi ya uchunguzi wa kisayansi pamoja na  chuo 
 • 14

Picha ya mlima Rungwe  mrefu kuliko yote Mbeya
Mlima Rungwe ndio mlima mrefu kuliko yote mjini Mbeya,
una urefu wa Takribani Mita 2960,
Foresti • Ghana • Iduda • Iganjo • Iganzo • Igawilo
Ilemi • Ilomba • Isanga • Isyesye • Itagano • Itende • Itezi •
Itiji • Iwambi • Iyela • Iyunga • Iziwa • Kalobe • Maanga •
Mabatini • Maendeleo • Majengo • Mbalizi Road • Mwakibete •
Mwansekwa • Mwansanga • Nonde • Nsalaga • Nsoho • Nzovwe •
Ruanda (Mbeya) • Sinde • Sisimba • Tembela • Uyole9
 - Mkuu wa Mkoa
Abbas Kandoro
63,617 km²
 
Mheshimiwa wa Raisi wa Tanzania /Mbeya City (Mh J.K Nyerere)
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Abbas Kandoro

Mbunge wa Mbeya Mjini, Mh Joseph Mbilinyi,

Mungu ibariki Mbeya city/ Mungu Ibariki Tanzania


Friday, May 10, 2013

ZISOME SIRI 25 NZITO USIZOZIJUA KUHUSU MTANGAZAJI STANLAUS LAMBAT A.K.A BIG SHOW KUTOKA MBEYA CITY
JINA KAMILI; Stanslaus .S. Lambat
A.KA; Taryx, Big Show,

HOME; Mbeya City
TAREHE YA KUZALIWA; 26/10/1989
SHULE YA MSINGI;  Msewe Primary. & Maanga
SHULE YA SEKONDARI; Mbeya day Secondary School
UMEOA; HAPANA
UNA MCHUMBA; HAPANA (Am Looking for her)
MUZIKI UNAOUPENDA: Hip hop,na kila aina ya Muziki Mzuri.
KIPAJI;Utangazaji,

Lambat akiwa katika kwa ofis Mbeya Fm akifanya yake

KAZI YAKO YA KWANZA; Producer  pia nmewahi kuwa Mwandishi wa
 Speech's na Mashairi
KIPAJI KINGINE NJE YA UTANGAZAJI: Pool table, Football
KAZI  NYINGINE NJE YA UTANGAZAJI;  Promotion & Marketing Manager
 wa The Vibe Club-Mbeya
REDIO NGAPI UMESHAWAHI TANGAZA; Mbeya Fm pekee
NANI ALIYEKUVUTIA KUWA MTANGAZAJI HAPA TANZANIA: Taji Liundi
NANI ALIYEKUVUTIA KUWA MTANGAZAJI NJE YA TANZANIA: Jina limenitoka\

 Huyu ndie mtangazaji ambaye Stanslaus lambat anamkubali sana

UNAKOISHI; ahahah unataka kuja kupiga chabo nini siku moja.?
 Ok mi nakaa Uhindini Katikati ya jiji la Mbeya tu.!
NDOTO ZAKO ZA BAADAE; Kuwa na Mafanikio Makubwa sana
UNAPENDA SIASA; Yes, lakini siishi ndani ya Siasa (hususani siasa chafu)
NI CHAMA GANI UNAKIPENDA; Sina Chama
MCHEZO UNAOUPENDA; Mieleka

 Undertaker ndie mwanamieleka ambaye Huwa kipaji
 chake humvutia mno Stanslaus Lambat

TIMU YA NJE NA NDANI UNAYOI SHABIKIA; Man U & Simba Fc

 Simba Sc au Mnyama na Manchester united ndizo timu ambazo
 Stanslaus Lambat huzishabikia

KITU USICHOKIPENDA ZAIDI; Dharau,Uongo na Unafiki
KITU UNACHOKIPENDA ZAIDI; Uwazi,Ukweli na Kila Jambo zuri


Kwa upande wa Tanzania Mwanadada mwasiti ndie humkosha
zaidi Lambat kwa upande wa wanaume Mwanafalsasa OR MwanaFA ndie 
Humkosha Lambat

Jigga Man Or Jay Z pichani juu
na Lady Gaga ndio wanamuziki ambao humvutia zaidi 
Stanslaus Lambat kwa upande wa nje ya TanzaniaStanslaus Lambat ktk picha tofauti akiwa na Rafiki zake
mbali mbali maeneo ya Green City

UNADHANI KITENDO WATANGAZAJI WASANII WANAOUKIMBIA
 MKOA WA MBEYA NA KWENDA NJE YA MKOA KINA MANUFAA 
YEYOTE KWA JIJI LA MBEYA;?-
Manufaa yapo maana bado wanaitangaza 
Mbeya na hutupatia namna ya kupenyeza Mazao ya Mbeya kupitia wao...!!
 Ingawa kuna wakati Maslahi ni Muhimu kwao, maana
 huwezi kujua kwann wanahama

UNA USHAURI GANI KWA RAISI J.K MRISHO KIKWETE
 NA MBUNGE JOSEPH MBILINYI;? - 

Mheshimiwa J.K Kikwete Namshauri aendelee kukaza buti tu,
 though ni Muhimu atazame wasaidizi wake kwa Jicho la Tatu..

Pia Mp Sugu namshauri aendelee kukomaa tu na akaze buti haswa
 Maana Mbeya inamuamini.! 

comments

***